Kanisa Dogo la Kuabudu Damu Azizi ya Yesu (Adoration Chapel)
Okt242026
Tukio

Kanisa Dogo la Kuabudu Damu Azizi ya Yesu (Adoration Chapel)

Kanisa dogo la Mt. Gaspar la kuabudu Damu Azizi ya Yesu kwa ukimya: mahali pa amani pa kusali, kusoma Biblia, kusali Rozari na kutulia mbele ya Bwana.

Tarehe ya tukio 24 Okt 2026 Jumamosi
MahaliParokia ya Mt. Gaspar del Bufalo, Mbezi Beach
Muda wa kusoma Dakika 2 za kusoma

Hili ni kanisa dogo la kuabudia Damu Takatifu ya Bwana wetu Yesu Kristo.

Ni mahali pa amani kubwa, pasipo mazungumzo wala kelele, ili kila mtu apate nafasi ya kusali na kutafakari moyoni mwake.

KUSALI BINAFSI
Watu huenda hapo kusoma Biblia, kusali Rozari, au kukaa kimya tu mbele ya Yesu, wakimweleza shida zao na kumshukuru. Waamini huabudu kwa ukimya na utulivu, wakijipatanisha na Mungu.

HADHI YA PEKEE
Kanisa hili limeipa Parokia ya Mt. Gaspar del Bufalo na Kituo cha Hija hadhi kubwa, kwa kuwa ndicho kituo pekee cha kuabudia Damu Takatifu ya Bwana wetu Yesu Kristo katika Tanzania nzima na Afrika.

KUABUDU NI NINI?
Kuabudu ni kumtambua Mungu kuwa ni Mungu, na kumpa heshima, upendo na shukrani. Katika kanisa hili tunamwabudu Yesu Kristo, aliyetukomboa kwa Damu yake Azizi iliyomwagika msalabani, na ambaye yupo kweli katika Ekaristi Takatifu.

JINSI YA KUTEMBELEA
• Ingia kwa utulivu, na upige magoti au uiname kwa heshima mbele ya Bwana.
• Zima simu yako au iweke kimya, na epuka mazungumzo ndani ya kanisa.
• Tumia muda wako kusali: soma Biblia, sali Rozari au Rozari ya Damu Azizi, au kaa kimya tu mbele ya Bwana.
• Waombee pia wengine: familia yako, wagonjwa na parokia yetu.
• Ukiwa hapa, tembelea pia Vituo vya Hija vilivyopo katika viwanja vya parokia.
• Toka kwa utulivu ili usiwasumbue wengine wanaosali.

Karibu ukae na Yesu. "Je! Hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja?" (Mathayo 26:40)

Maelezo Zaidi

Hii ni Altare ndogo, ambayo pia hutumika kuadhimishia ibada ya Misa Takatifu kwa heshima ya Mt. Gaspar del Bufalo.

Mahali hapa pana kaburi la Mt. Gaspar del Bufalo na masalia yake; waumini husali mahali hapa kwa heshima ya Mt. Gaspar del Bufalo.

Altare ya Mt. Gaspar del Bufalo

Hii ni Altare kuu, ambayo hutumika kuadhimishia ibada ya Misa Takatifu kila Jumapili na sikukuu za Kanisa.

Ni Altare iliyowekwa maalum kwa ajili ya kuadhimisha sadaka kuu ya Bwana wetu Yesu Kristo, ambapo mkate na divai hugeuzwa kuwa Mwili na Damu yake.

Ndani ya Altare hii pia yamewekwa masalia ya Mtakatifu wa Parokia (Mt. Gaspar del Bufalo).

Altare Kuu

Hii ni Altare ndogo kanisani, ambayo hutumika kuadhimishia ibada ya Misa Takatifu kwa heshima ya Moyo Mtakatifu wa Yesu.

Sherehe ya Moyo Mtakatifu wa Yesu huadhimishwa Ijumaa ya kwanza inayofuata Sherehe ya Mwili na Damu ya Bwana (Corpus Christi), na mara nyingi huangukia mwezi Juni, kulingana na kalenda ya Pasaka.

Altare ya Moyo Mtakatifu wa Yesu