Habari za Kanisa
Current News

Kongamano la vijana Roma Mwaka 2025 Mahujaji wa matumaini
Waamini wote wanapaswa kwenda vituo vya hija mwaka huu iwe ndani au nje ya nchi. Watoke kushiriki kauli mbiu hii kwa vitendo kupitia sala.

TUNAYE PAPA MPYA
Papa Leo XIV, O.S.A. (jina la kuzaliwa: Robert Francis Prevost, alizaliwa 14 Septemba 1955) ni kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki na Mtawala wa Mji wa Vatikani. Alichaguliwa kuwa Papa tarehe 8 Mei 2025 kufuatia kifo cha Papa Fransisko. Ndiye Papa wa kwanza kutoka Marekani na Amerika ya Kaskazini kwa ujumla[1]. Akiwa mtawa wa Shirika la Mtakatifu Augustino (O.S.A.), aliwahi kuhudumu katika nyadhifa za juu ndani ya shirika hilo na ndani ya ofisi kuu za Kanisa, zikiwemo Mkuu wa Idara ya Maaskofu na Rais wa Tume ya Kipapa kwa Amerika ya Kilatini

Jubilei 2025 Mahujaji wa matumaini
Waamini wote wanapaswa kwenda vituo vya hija mwaka huu iwe ndani au nje ya nchi. Watoke kushiriki kauli mbiu hii kwa vitendo kupitia sala.