Matangazo ya Jumapili 25 Oktoba
Jubilei ya Miaka 75 ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam: Tufanywe upya na Roho Mtakatifu!
-
Leo ni Dominika ya 30 ya mwaka A wa Kanisa. Pia ni Sherehe ya Somo wa Parokia.
-
Dominika ijayo ni Dominika ya 31 ya mwaka A wa Kanisa.
-
USAFI na usimamizi ni zamu ya JNNK zifuatazo:
MISA JNNK 1. MISA YA KWANZA Mt. Margaretha Maria 2. MISA YA PILI Bikira Maria Mama wa Damu Azizi 3. MISA YA TATU Mt. Yuda Thadei 4. MISA YA NNE Karismatiki Katoliki Telezesha pembeni kuona jedwali lote -
Tunawashukuru wote waliofanya USAFI jana Jumamosi na kutoa huduma kanisani: Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni walikuwa 01, Damu Azizi ya Yesu walikuwa 15 na Mt. Fransis wa Assisi walikuwa 11. Jumuiya zote zilitoa mchango wa mapambo. Mwenyezi Mungu awabariki nyote kwa majitoleo yenu.
-
Leo ni SHEREHE YA SOMO WA PAROKIA (GASPAR DEL BUFALO DAY). Kutakuwa na Misa tatu asubuhi; Misa kuu itaanza saa 3:30 asubuhi.
Kutakuwa na uzinduzi wa Jubilei ya Miaka 75 ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam ngazi ya Parokia, kuzinduliwa kwa VIWAWA APP, na kupokelewa na kurudia ahadi kwa Wana Utume wa Damu Azizi.
-
Jumanne tarehe 27.10.2026 Baba Askofu Mkuu Jude Thaddeus Ruwaichi atapongezwa na Wanadekania wa Dekania yetu ya Mt. Thomas More kwa kutimiza miaka 50 ya utawa. Hivyo mwaliko utakuwa kwa ngazi ya vyama vya kitume, kila parokia waamini 35:
CHAMA CHA KITUME WAAMINI i. Uwaka 3 ii. Wawata 3 iii. Wazee na wastaafu 3 iv. Viwawa 3 v. Ushirika wa Moyo Mt. 2 vi. Utume wa Damu 2 vii. Utume wa Fatima 2 viii. Legio Maria 2 ix. Shirika la Mt. Anna 2 x. Karismatiki Katoliki 2 xi. Rozari Hai 2 xii. Watangaza Neno 2 xiii. Walezi wa Utoto 2 xiv. Kamati Tendaji Parokia 5 Telezesha pembeni kuona jedwali lote -
Shule ya Awali na Msingi Josephine Bakhita iliyoko Tegeta kwa Ndevu itakuwa na mtihani wa kujiunga na madarasa mapya 2027 Jumamosi ijayo tarehe 31.10.2026 kuanzia saa 2 asubuhi. Fomu na maelezo zaidi yanapatikana shuleni.
-
Karismatiki Katoliki wameandaa Maombi ya siku 10 yatakayoongozwa na Fr. Mapinduzi kuanzia tarehe 01.11.2026 hadi 10.11.2026; muda ni saa 9 hadi saa 12 jioni.
-
Makusanyo ya Wiki: (Yasomwe)
-
Matangazo ya ndoa: (Yasomwe kama yapo)