Rudi Nyumbani
Alhamisi, 29 Oktoba 2026
Ubao wa Matangazo ya Parokia

Matangazo ya Kanisa

Matangazo 10 yanayoendelea, yamepangwa kipengele kwa kipengele.

25 Okt 2026 Vipengele 10

Matangazo ya Jumapili 25 Oktoba

Jubilei ya Miaka 75 ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam: Tufanywe upya na Roho Mtakatifu!

  1. Leo ni Dominika ya 30 ya mwaka A wa Kanisa. Pia ni Sherehe ya Somo wa Parokia.

  2. Dominika ijayo ni Dominika ya 31 ya mwaka A wa Kanisa.

  3. USAFI na usimamizi ni zamu ya JNNK zifuatazo:

    MISAJNNK
    1.MISA YA KWANZAMt. Margaretha Maria
    2.MISA YA PILIBikira Maria Mama wa Damu Azizi
    3.MISA YA TATUMt. Yuda Thadei
    4.MISA YA NNEKarismatiki Katoliki
    Telezesha pembeni kuona jedwali lote
  4. Tunawashukuru wote waliofanya USAFI jana Jumamosi na kutoa huduma kanisani: Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni walikuwa 01, Damu Azizi ya Yesu walikuwa 15 na Mt. Fransis wa Assisi walikuwa 11. Jumuiya zote zilitoa mchango wa mapambo. Mwenyezi Mungu awabariki nyote kwa majitoleo yenu.

  5. Leo ni SHEREHE YA SOMO WA PAROKIA (GASPAR DEL BUFALO DAY). Kutakuwa na Misa tatu asubuhi; Misa kuu itaanza saa 3:30 asubuhi.

    Kutakuwa na uzinduzi wa Jubilei ya Miaka 75 ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam ngazi ya Parokia, kuzinduliwa kwa VIWAWA APP, na kupokelewa na kurudia ahadi kwa Wana Utume wa Damu Azizi.

    Jumapili, 25 Okt 2026 9:30 AM Parokia ya Mt. Gaspar del Bufalo
  6. Jumanne tarehe 27.10.2026 Baba Askofu Mkuu Jude Thaddeus Ruwaichi atapongezwa na Wanadekania wa Dekania yetu ya Mt. Thomas More kwa kutimiza miaka 50 ya utawa. Hivyo mwaliko utakuwa kwa ngazi ya vyama vya kitume, kila parokia waamini 35:

    Jumanne, 27 Okt 2026
    CHAMA CHA KITUMEWAAMINI
    i.Uwaka3
    ii.Wawata3
    iii.Wazee na wastaafu3
    iv.Viwawa3
    v.Ushirika wa Moyo Mt.2
    vi.Utume wa Damu2
    vii.Utume wa Fatima2
    viii.Legio Maria2
    ix.Shirika la Mt. Anna2
    x.Karismatiki Katoliki2
    xi.Rozari Hai2
    xii.Watangaza Neno2
    xiii.Walezi wa Utoto2
    xiv.Kamati Tendaji Parokia5
    Telezesha pembeni kuona jedwali lote
  7. Shule ya Awali na Msingi Josephine Bakhita iliyoko Tegeta kwa Ndevu itakuwa na mtihani wa kujiunga na madarasa mapya 2027 Jumamosi ijayo tarehe 31.10.2026 kuanzia saa 2 asubuhi. Fomu na maelezo zaidi yanapatikana shuleni.

    Jumamosi, 31 Okt 2026 8:00 AM Shule ya Josephine Bakhita, Tegeta kwa Ndevu
  8. Karismatiki Katoliki wameandaa Maombi ya siku 10 yatakayoongozwa na Fr. Mapinduzi kuanzia tarehe 01.11.2026 hadi 10.11.2026; muda ni saa 9 hadi saa 12 jioni.

    Jumapili, 1 Nov 2026 3:00 PM
  9. Makusanyo ya Wiki: (Yasomwe)

  10. Matangazo ya ndoa: (Yasomwe kama yapo)